Reputation Management
CPR certification onlineCPR certification online

Mazoezi kama kitendo muhimu kwa afya na maisha yetu, yanatakiwa kufanyika kwa usahihi na katika mazingira yanayokubalika. Wengi wetu hupuuzia vitu hivi ambavyo huonekana si muhimu na mwisho wa siku kutufanya tusifaidike na mazoezi tuyafanyayo . Lakini pia, ziko imani potofu zinazopelekea kutokuzingatia vifaa na mazingira sahihi kwa mazoezi kitu ambacho huweza kutusababishia kuumia na majeraha. Leo tunajadili imani nne (4) potofu kuhusu mazoezi zilizoenea sana hapa nchini

1. Kuvaa nguo za joto wakati unapofanya mazoezi

Kupandisha sana joto wakati wa mazoezi kwaweza kuathiri afya yako

Ni kawaida kabisa kukutana na mtu akiwa anakimbia huku amevalia jaketi au koti lenye kofia kichwani, hata katika kipindi cha joto kali. Wengi huamini kwamba kwa kufanya hivyo wanatoa jasho jingi na kuchoma nishati lishe (calories) nyingi zaidi hivyo kupungua uzito kiurahisi.

Kwa kifupi hii ni imani potofu na kitendo hicho chaweza kuhatarisha afya yako. Chimbuko la imani hii potofu limetokana na matumizi mabaya ya teknolojia. Watu wengi hupata muongozo wa mazoezi kutoka katika tovuti ambazo walengwa wake ni watu wanaoishi katika nchi au mazingira yenye baridi sana. Kwa kutazama filamu zilizotengenezwa katika nchi hizo pia, watu huiga kile kinachofanyika katika mazingira hayo na kudhani ni chenye faida katika mazingira yetu ya joto.

Kumbuka kwamba kupandisha sana hali ya joto ya mwili wakati wa mazoezi huweza kukusababishia kuchoka, kupoteza maji mengi na hata kuufanyisha moyo wako kazi ya ziada isiyo na tija.

Lakini ifahamike kwamba kufanya hivi kunaweza kuwapa faida wanamichezo wanaojiandaa kufanya pambano kwenye nchi zenye joto zaidi kuliko hapa kwetu. Mfano bondia au mwanariadha ana mashindano nchini Misri; kufanya mazoezi katika mazingira ya joto ni kama kujiandaa na mazingira hayo.

2. Kufanya mazoezi kwenye mazingira ya joto na yasiyo na mzunguko mzuri wa hewa

Mazoezi ya ndani yanapaswa kufanyika kwenye chumba chenye nafasi, mwanga na mzunguko wa hewa wa kutosha

Hii haijanitokea mara moja. Kutofautiana na mwenzangu tunayejikuta tunafanya mazoezi katika sehemu yenye kipooza joto (AC) kutokana na yeye kutaka tuzime kipooza joto hicho.

Kama nilivyoelezea kuhusiana na nguo za joto, kutengeneza mazingira feki yatakayokufanya utokwe jasho haraka hakukusaidii chochote katika kupunguza uzito au kupata faida zingine kiafya.

Kimsingi, kufanya mazoezi katika chumba chenye joto huongeza hali ya unyevu nyevu (humidity) kitu ambacho hukufanya uchoke mapema. Lakini pia kufanya hivi hupandisha mapigo yako ya moyo haraka sana na kutumia akiba yako ya nguvu. Katika sehemu zenye joto kama Dar es salaam, mazoezi ya ndani ni sharti yafanyike katika sehemu zenye vipoza joto (AC) na hewa ya kutosha, endapo sehemu hizo haziko wazi. Ikumbukwe kwamba siyo kupoteza jasho ndo kunakokufanya ufaidike na mazoezi, bali kiasi cha juhudi ambazo hukufanya utokwe jasho.

3. Kufanya mazoezi ya aerobics peke yake ili kupunguza mafuta mwilini

Mazoezi ya aerobics husita kufanya kazi pale tu unapomaliza kufanya mazoezi

Hili tumeshalijadili mara nyingi. Ipo imani, hususani kwa kina dada na kina mama kwamba mazoezi ya kunyanyua na kusukuma uzito au mazoezi ya nguvu (resistance exercises) ni kwa ajili ya watunisha misuli, wapiganaji ngumi na wanaume peke yao. Hii ni imani potofu na ni sababu kubwa ya watu wengi kushindwa kufikia malengo yao ya kupunguza mafuta mwilini.

Unapofanya mazoezi ya aerobics kama vile kukimbia, mwili wako unachoma mafuta kipindi unachofanya mazoezi. Mwili huo husita kuchoma mafuta pale tu unapomaliza kufanya mazoezi. Lakini unapofanya mazoezi ya nguvu (resistance) kwa kuvuta au kusukuma uzito, mwili wako utaendelea kuchoma mafuta kwa takribani masaa arobaini na nane (48) baada ya kuacha kufanya mazoezi.

Maana yake ni kwamba, mwili wako utakuwa na uwezo wa kuendelea kuchoma mafuta kwa siku mbili zaidi baada ya wewe kuacha kufanya mazoezi. Ili kuchoma mafuta ipasavyo, na kupunguza mafuta mwilini, inashauriwa kuchanganya mazoezi ya aerobics na yale ya kutumia nguvu.

4. Viazi mviringo ni bora kuliko viazi vitamu kwa kupunguza mafuta mwilini

Elimu ya lishe ni muhimu sana katika kutimiza malengo na kufaidika na mazoezi

La hasha, hakuna ukweli katika hilo. Imani hii hutokana na hisia na logic vitu ambavyo kisayansi havina nafasi kabisa. Wengi wetu hudhani kwamba, kutokana na viazi vitamu kuwa na sukari (vitamu), basi ni dhahiri kwamba kiafya vitakuwa na madhara kuliko vile vya mviringo. Tafiti za kisayansi na zile za kijamii zimeonyesha tofauti. Hii inatokana na ukweli kwamba sukari iliyo katika viazi vitamu huingia kwenye damu taratibu zaidi ya ile kidogo inayopatikana kwenye viazi mviringo. Kitendo cha sukari kuingia kwa kasi katika damu husababisha kutengenezwa kwa kiasi kikubwa cha homoni ya insulin, ambayo kazi yake kwa kisi kikubwa ni kutunza virutubisho. Kiasi kikubwa cha virutubisho kinachotunzwa mwilini, ndiyo hutufanya kuongezeka mafuta. Kupunguza mafuta mwilini, vifanye viazi vitamu view mbadala wa viazi mviringo.

 

Free Presentantion on ...

Free Presentation on Weight Loss with Zohra ...

+ View

Recent Articles

MEN’S BELLY FAT: Pride ...

The fact that abdominal fat, or belly fat, is not ...

+ View

Kuondoa kitambi, tumia ...

Nadhani katika kitu ambacho wengi wanapambana ...

+ View

Ushauri wa mazoezi kwa ...

Ni kawaida kwa watu wenye umri wa miaka 50 na ...

+ View
  • Prev
  • Sponsor this Section
Scroll to top