Reputation Management
CPR certification onlineCPR certification online

 

Nini cha kuzingatia? 

Tayari tunafahamu umuhimu wa mazoezi katika kudumisha afya na kuzuia magonjwa mbalimbali. Tunafahamu pia mazoezi ni sehemu muhimu ya matibabu au udhibiti wa magonjwa chungu nzima ikiwemo tatizo la kupanda kwa shinikizo la damu. Kupanda kwa shinikizo la damu au high blood pressure ni ugonjwa unaongezeka kwa kasi sana katika Jamii yetu. Kupanda kwa shinikizo la damu huweza kusababisha madhara kama vile shambulio la moyo, kufeli kwa moyo kufanya kazi, kiharusi na hata upofu.

Japo ya mazoezi kuwa sehemu muhimu ya matibabu ya tatizo hili, yako mambo muhimu ya kuzingatia kabla, wakati na baada ya kuanza programu yeyote ya mazoezi inayomlenga mtu mwenye tatizo la kupanda kwa shinikizo la damu.

1. Zungumza na daktari wako kuhusu umuhimu wa mazoezi

Ni muhimu kuzungumza na daktari kabla ya kuanza programu ya mazoezi

Ni muhimu sana kujadili na daktari wako kwa kina kuhusu umuhimu na jinsi ya kuanza mazoezi. Hii hutokana na ukweli kwamba uwepo wa tatizo hili hutofautina kati ya mtu na mtu. Kuna watu ambao kiwango cha kupanda kwa shinikizo lao la damu hakimruhusu kufanya mazoezi kabisa au hakimruhusu kufanya mazoezi ya aina fulani. Kwa kujadiliana na daktari wako utapata ufahamu kuhusu mambo yote hayo

2. Fanya vipimo vyote muhimu mara kwa mara

Fanya vipimo vyote muhimu

Ni muhimu kufanya vipimo vyote kama unavyoshauriwa na daktari. Hii itakusaidia kufahamu aina, kiwango na muda wa kufanya mazoezi ili kupata faida zaidi na kukwepa kupata madhara ya aina yeyote.

3. Pima shinikizo la damu kabla ya kuanza mazoezi

Pima shinikizo la damu kabla ya kuanza mazoezi

Ifahamike kwamba mazoezi hupandisha shinikizo la damu. Maana yake ni kwamba endapo shinikizo lako lilikuwa juu sana kabla ya kuanza ni hatari kufanya mazoezi. Kufanya mazoezi wakati shinikizo lako la damu liko juu, kutasababisha shinikizo hilo kupanda zaidi kitu ambacho kinaweza hata kukusababishia kiharusi au stroke.

5. Kuwa muangalifu unapofanya mazoezi ya kusukuma/kunyanyua uzito

Mazoezi ya kusukuma/kunyanyua uzito au resistance exercise yanatakiwa kufanywa kwa uangalifu sana kwa watu wenye tatizo hili. Hii inatokana na ukweli kwamba mazoezi haya huongeza ukinzani katika mishipa ya damu kitu ambacho huongeza shinikizo la damu kwa kiasi kikubwa sana. Hii haimanishi mazoezi haya yasifanyike, bali yafanyike kwa uangalifu na ikiwezekana yafuate maelekezo ya mtaalamu wa mazoezi

6. Zingatia kiwango chako cha juu kabisa cha kasi ya mapigo ya moyo unapofanya mazoezi (maximum heart rate)

Fahamu kiwango cha juu kabisa cha kasi ya mapigo ya moyo wako

Unapofanya mazoezi kama vile kukimbia, kasi ya mapigo ya moyo huongezeka kutokana na kasi au kiwango cha mazoezi. Mioyo yetu inaweza kuhimili kasi ya mazoezi mpaka kiwango fulani kwa kuongeza kasi yake ya kusukuma damu. Kiko kikomo cha uwezo wa moyo kufanya hivyo kwa maana kwamba ukiongeza kasi ya mazoezi ziada ya uwezo wa moyo wako unakuwa unahatarisha afya yako. Uwezo wa moyo wako kukabiliana na kasi au viwango vya mazoezi hutegemeana na umri wako.

Unaweza kufahamu kiwango cha juu kabisa cha kasi ya moyo wako kwa kuchukua namba 220 kutoa umri wako (220-umri). Kwa kawaida tunashauriwa kufanya mazoezi kiasi cha mapigo yetu ya moyo kufikia kati ya asilimia hamsini (50%) mpaka themanini na tano (85%) ya kiwango cha juu kabisa cha kasi za mapigo hayo (50-85% of maximum heart rate).

Free Presentantion on ...

Free Presentation on Weight Loss with Zohra ...

+ View

Recent Articles

MEN’S BELLY FAT: Pride ...

The fact that abdominal fat, or belly fat, is not ...

+ View

Kuondoa kitambi, tumia ...

Nadhani katika kitu ambacho wengi wanapambana ...

+ View

Ushauri wa mazoezi kwa ...

Ni kawaida kwa watu wenye umri wa miaka 50 na ...

+ View
  • Prev
  • Sponsor this Section
Scroll to top