Reputation Management
CPR certification onlineCPR certification online

Kujenga au kudumisha misuli ni mada maarufu kwa watunisha misuli, wacheza mieleka na kwa kiasi fulani, kwa wanaume. Hivi ndivyo tulivyozoea. Hata mazoezi ya nguvu (kunyanyua/kuvuta/kusukuma vitu vizito) au resistance exercises huonekana kama mazoezi ya watunisha misuli au wanaume peke yao. Leo nataka nikuamshe kwa kukufahamisha kwamba, misuli ni muhimu kwa afya ya kila mmoja wetu.

Ni vyema kufahamu kwamba miili yetu huanza kupoteza misuli tunapofikia umri wa miaka 25. Kiasi cha misuli inayopotea au kupukutika kutoka katika miili yetu huongezeka mara dufu tunapofikia miaka kati ya arobaini (40) na hamsini (50). Hii huchangia kwa kiasi kikubwa katika kusababisha matatizo ya afya yanayotokana na umri mkubwa.

Kutokana na ukweli huo wa kibaiolojia usiopingika, ni dhahiri kwamba tunahitaji kufanya juu chini ili kudumisha kiwango cha misuli katika miili yetu.

Pamoja na kupata lishe muafaka, kufanya mazoezi ya kusukuma/kunyanyua/kuvuta uzito au kwa lugha ya kitaalamu resistance exercises ni njia madhubuti ya kudumisha au kuongeza kiasi cha misuli mwilini. Katika makala zijazo tutajadili undani wa mazoezi ya aina hii, pamoja na kupata ufahamu wa lishe inayosaidia kudumisha au kujenga misuli. Leo tujikite zaidi katika kufahamu umuhimu wa misuli kwa afya zetu.

1. Misuli husaidia kuchoma mafuta

Misuli inauwezo mkubwa wa kuchoma mafuta mwilini

Kwa kifupi kiasi kikubwa cha mafuta huchomwa katika misuli. Kadri kiasi cha misuli kinavyopungua, ndivyo miili yetu hushindwa kuchoma mafuta. Hii ndiyo husababisha ugumu wa kupambana na mafuta mwilini pale tunapofikia miaka 25 na kuendelea.

2. Misuli husaidia kuzuia ugonjwa wa kisukari

Sehemu kubwa ya sukari itokanayo na chakula hutumiwa kwenye misuli

Zaidi ya asilimia 70 ya sukari itokanayo na chakula tunachokula,huingia na kutumiwa kwenye misuli. Hii inamaana kwamba kutokuwa na kiwango cha kutosha cha misuli huifanya miili yetu ishindwe kutumia sukari ipasavyo, kitu ambacho husababisha sukari kuongezeka katika damu. Sukari kuongezeka katika damu ndiyo sifa kuu ya ugonjwa wa kisukari. Chama cha kisukari cha nchini Marekani (ADA) kinawashauri watu wanaoishi na ugonjwa wa kisukari kufanya mazoezi ya kubeba/kuvuta/kusukuma vitu vizito angalau mara mbili kwa wiki. Hii huwasaidia kuongeza au kudumisha kiasi cha misuli miilini mwao, ili miili hiyo iweze kutumia sukari ipasavyo.

3. Misuli hukupa nguvu na uwiano (balance)

Balance ni muhimu kuzuia kuanguka mara kwa mara

Misuli ndiyo kiwanda kikuu cha nguvu mwilini. Halikadhalika misuli hutupa uwiano au balance kitu ambacho hutuwezesha kujongea na kufanya kazi kwa ufasaha. Moja wapo ya tatizo linalowakumba watu wenye umri mkubwa ni pamoja na kukosa balance na kuanguka mara kwa mara. Hii hutokana na hali ya kutokuwa na kiwango/kiasi halisi cha misuli ambayo husababisha kukosa nguvu na uwiano/balance hivyo kuanguka mara kwa mara.

4. Kudumisha na kuongeza misuli husababisha uimarishwaji wa mifupa

Mazoezi ya resistance husaidia kuimarisha misuli na mifupa

Mazoezi ya resistance, ambayo husaidia kudumisha kiwango/kiasi cha misuli, husaidia pia kuimarisha mifupa. Kwa maana hiyo juhudi za kujenga misuli hutusaidia kuimarisha mifupa na kuipa nguvu.

5. Misuli husaidia kudumisha kiwango cha vichocheo muhimu mwilini

Kichocheo/homoni ya testosterone hupungua kadri kisi cha misuli kinavyopungua mwilini

Kiwango cha homoni ya kiume au testosterone hupungua mwilini kadri kiasi cha misuli kinavyopungua. Kufanya mazoezi ya resistance husaidia kuzuia kupungua kwa kasi kwa kichocheo hiki kutokana na uwezo wa mazoezi haya kuzuia upoteaji wa misuli utokanao na umri mkubwa.

Free Presentantion on ...

Free Presentation on Weight Loss with Zohra ...

+ View

Recent Articles

Utastaajabishwa na ...

Wakati mwingine tunakata tamaa kufanya mambo ...

+ View

Matatizo sugu yanayo ...

Wengi wetu tunafahamu umuhimu wa mazoezi katika ...

+ View

MEN’S BELLY FAT: Pride ...

The fact that abdominal fat, or belly fat, is not ...

+ View
  • Prev
  • Sponsor this Section
Scroll to top