Reputation Management
CPR certification onlineCPR certification online

Wakati mwingine tunakata tamaa kufanya mambo fulani kwa kukosa sababu zinazo tupelekea kufanya mambo hayo. Na mara nyingi tunakosa sababu kutokana na kutokuwepo kwa shahidi za kitaalamu zinazo tuhamasisha kufanya hivyo. Leo tutafanya angalizo na kuchambua matokeo ya tafiti kubwa kabisa duniani kuhusu umuhimu wa mazoezi katika maisha na kwa afya zetu.

1. Watu wanao fanya mazoezi mara kwa mara, wana uwezekano mdogo zaidi wa kupoteza maisha kunako sababishwa na matatizo mbalimbali

Mazoezi hutukinga na vifo vinavyoweza kusababishwa na magonjwa mbali mbali

Katika utafiti uliohusisha wanaume na wanawake wa umri wa kati, ambapo watu hawa walifuatiliwa kwa muda wa takribani mika nane (8), ilionekana kwamba, ukilinganisha na wale wasiofanya mazoezi, wengi wa wanawake na wanaume waliokuwa wakifanya mazoezi mara kwa mara hawakupoteza maisha yao katika kipindi hicho cha miaka nane. Hii inamaana kwamba kundi kubwa la waliopoteza maisha lilitoka katika kundi la watu wasiofanya mazoezi.

Tafiti za hivi karibuni zimedhihirisha umuhimu huu wa mazoezi kwa kuonyesha kwamba, watu wasio fanya mazoezi mara kwa mara wana uwezekano mkubwa wa kupoteza maisha mara mbili zaidi ya wale wanao fanya mazoezi mara kwa mara.

2. Kufanya mazoezi mara kwa mara kunaweza kupunguza makali na kuzuia vifo kwa watu wenye magonjwa ya moyo

Unaweza kuepuka vifo vinavyoweza kusababishwa na maradhi ya moyo kwa kufanya mazoezi

Mnyumbulisho wa muunganisho wa matokeo wa tafiti zaidi ya 48 (meta-analysis) zilizofanyika katika sehemu mbalimbali za dunia unaonyesha kwamba, kufanya mazoezi mara kwa mara huweza kupunguza makali na hata kuponya baadhi ya maradhi yanayoombatana na magonjwa ya moyo. Mnyumbulisho huu umeonyesha pia kwamba, watu wenye maradhi ya moyo na mfumo wa mishipa ya damu (cardiovascular diseases) waliokuwa wakifanya mazoezi mara kwa mara, walijikinga na vifo vya mapema vinavyoweza kusababishwa na maradhi hayo.

Tafiti zinatuonyesha kwamba japo mazoezi hufanya kazi vizuri zaidi katika kuzuia magonjwa, mazoezi pia yanao mchango mkubwa katika kuponya magonjwa hayo.

3. Mazoezi ya kasi (aerobics) na yale ya nguvu (resistance) husaidia kuzuia ugonjwa wa kisukari

Kutokana na tafiti, mazoezi ya kasi na yale ya nguvu hutuepusha na ugonjwa wa kisukari

Matokeo ya utafiti mkubwa uliohusisha madaktari wa kiume takribani 21,000 huko nchini marekani umebaini kuwa, asilimia kubwa ya madaktari waliokuwa wakifanya mazoezi ya kutosha kutoa jasho kila mara, hawakupata ugonjwa wa kisukari ukilinganisha na wale wasiofanya mazoezi. Mazoezi haya yalihusisha yale ya kasi (aerobics) na hata yale ya kutumia nguvu (resistance). Faida hizi chanya zilionekana zaidi katika kundi la watu wenye uzito mkubwa ambao ki uhalisia wana hatari kubwa zaidi wa kupatwa na ugonjwa huo. Hii inamaana kwamba mazoezi huweza kuzuia ugonjwa wa kisukari hata kwa watu wenye uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa huo, ikiwemo wenye historia za tatizo hilo katika familia zao. Ziko tafiti chungu nzima zinazo shabiiana na utafiti huu.

Mnyambulisho wa muunganisho wa matokeo ya tafiti nyingi katika eneo hili umeonyesha pia kwamba kwa kufanya mazoezi mara kwa mara na kula lishe bora, watu wenye hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa kisukari wanaweza kuzuia ugonjwa huo kwa asilimia mpaka 60 (60%).

4. Mazoezi kama sehemu ya kazi, kusafiri au mazoezi maalumu huzuia saratani ya matiti na ile ya utumbo mpana.

Kutokana na tafiti, kuendesha baiskeli, kutembea na kufanya kazi za nyumbani kunaweza kukukinga na baadhi ya saratani

Mnyambulisho wa mkusanyiko wa matokeo ya tafiti zaidi ya 100 (meta-analysis) umeonyesha kwamba mazoezi ya wastani kama sehemu ya kazi, kusafiri au mazoezi maalumu huzuia saratani ya matiti na utumbo mpana kwa wanawake na wanaume.

Matokeo haya yanaonyesha kwamba kufanya mazoezi hata kwa jumla ya masaa mawili kwa wiki huleta faida hiyo. Mazoezi yaliyo sehemu za shughuli za kila siku ni kama vile kufanya usafi, kulima, kusukuma mashine na vitu vyote vinavyousisha kujongea wakati wa kazi. Mazoezi yaliyo sehemu ya usafiri ni kutembea na kuendesha baiskeli wakati mazoezi maalumu huusisha michezo na kwenda gym.

Kumbuka, kutokwa jasho si kipimo kizuri cha kiwango cha mazoezi katika nchi za joto. Katika hali ya kawaida, watu hutokwa jasho hata wakiwa wamelala. Kuwa makini na vipimo vinavyoshauriwa katika nchi za baridi, maana huenda visiwe sawa katika nchi za joto

Wengi wetu tunafahamu umuhimu wa mazoezi katika kulinda afya zetu. Licha ya ufahamu huo, huenda tukawa hatufahamu ni mazoezi yapi tufanye ili yafanye nini katika miili yetu. Leo tutajadili matatizo makubwa matano ya kiafya yanayoweza kutuandama na aina za mazoezi zinazofaa kukabiliana nayo.

Read more ...

Nadhani katika kitu ambacho wengi wanapambana nacho, wake kwa waume–ni tatizo la kuongezeka kwa mafuta katika sehemu za tumbo au kitambi. Juhudi zinatokana na ukweli kwamba kiafya, mafuta yanayokaa tumboni ndiyo yenye madhara makubwa zaidi kwa afya zetu. Wengine wanapambana kupata muenekano wanaoamini kuwa ni wa kuvutia zaidi. Iwe kwa kutamani afya au muonekano bora, kupambana na kitambi ni jambo jema.

Read more ...

Ni kawaida kwa watu wenye umri wa miaka 50 na kuendelea kuishi bila kufanya mazoezi yeyote. Katika utafiti uliofanyika nchini Tanzania mwaka 2012 (Tanzania STEPS survey), imebainika kwamba watu wengi walio katika kundi hili (miaka 50 na kuendelea) hawatimizi viwango vya mazoezi vinavyoshauriwa na shirika la afya duniani.

Read more ...

Free Presentantion on ...

Free Presentation on Weight Loss with Zohra ...

+ View

Recent Articles

Utastaajabishwa na ...

Wakati mwingine tunakata tamaa kufanya mambo ...

+ View

Matatizo sugu yanayo ...

Wengi wetu tunafahamu umuhimu wa mazoezi katika ...

+ View

MEN’S BELLY FAT: Pride ...

The fact that abdominal fat, or belly fat, is not ...

+ View
  • Prev
  • Sponsor this Section
Scroll to top