Reputation Management
CPR certification onlineCPR certification online

Kama kuna kitu muhimu na cha msingi sana ambacho watu wengi hukichukulia "powa" ni swala la lishe na mazoezi. Wakati mwingine unatamani mungu ashuke nakuwaeleza wanadamu ni jinsi gani alivyowapa uwezo wa kuchagua kitu cha kufanya na mlo wa kula, ili kufurahia maisha. Kinadharai wengi wetu tunaufahamu ukweli kwamba chakula chaweza kuwa sumu au dawa, kutokana na jinsi kitakavyotumika. Lakini kimatendo ni watu wachache sana hufuatilia na kuishi maisha kwa kuzingatia kula chakula bora.

Tafiti, uzoefu na shuhuda zinaonyesha kwamba kula vibaya huchangia sana katika kusababisha magonjwa kama vile kisukari, saratani na matatizo ya moyo. Tafiti na uzoefu vinatupa pia ushahidi wa uwezo wa lishe bora kudhibiti magonjwa hayo.

Katika kipindi cha takriban miaka mitano sasa nimekuwa nikifuatilia kundi kubwa la watu ambao walikutwa na dalili na viashiria vya kuwa na ugonjwa wa kisukari (Diabetes Mellitus) au ule wa kupanda kwa shinikizo la damu (hypertension) ambao kwa uamuzi na sababu zao binafsi, hawakutaka kuanza kutumia dawa. Kutokana na uamuzi wao huo ikabidi wazingatie kwa ukaribu sana masharti ya lishe na mazoezi. Japo ya kufahamu sayansi ya lishe katika kudhibiti magonjwa sugu, nimejifunza mambo mengi kutokana na kile nilichokiona katika kundi hili la watu walioamua kuzingatia lishe bora.

Ukweli ni kwamba lishe bora imekuwa dawa kwa watu hawa, na kutupa mtazamo chanya kuhusu umuhimu wa chakula bora katika kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza (non-communicable diseases).

Usingoje kuumwa, anza leo kuzingatia lishe bora. Ndani ya mwezi mmoja utakuwa umejifunza mambo makubwa kwa vitendo. Na utakubalina na mimi kwamba, lishe ni dawa.

Free Presentantion on ...

Free Presentation on Weight Loss with Zohra ...

+ View

Recent Articles

Utastaajabishwa na ...

Wakati mwingine tunakata tamaa kufanya mambo ...

+ View

Matatizo sugu yanayo ...

Wengi wetu tunafahamu umuhimu wa mazoezi katika ...

+ View

MEN’S BELLY FAT: Pride ...

The fact that abdominal fat, or belly fat, is not ...

+ View
  • Prev
  • Sponsor this Section
Scroll to top