Reputation Management
CPR certification onlineCPR certification online

Misingi inafanana, lakini hakuna programu moja inayoweza kufanya kazi kwa watu wote.

Si kila mtu anapendelea kuwa na umbo au muonekano mzuri, ila nina uhakika kwamba, kila mtu anapenda kuwa na AFYA NJEMA. Kuzuia ongezeko la mafuta mwilini kwa kula chakula bora na kufanya mazoezi ni sehemu muhimu katika kuboresha AFYA zetu.

 

Ifahamike kwamba, ongezeko la mafuta mwilini, siyo tu huathiri muonekano, bali pia hutuweka kwenye uwezekano wa kupata magonjwa yasiyo ambukizi”.

Baadhi ya magonjwa yanayoweza kusababishwa na ongezeko la mafuta mwilini ni pamoja na,KISUKARI, SHINIKIZO LA DAMU, MAGONJWA YA MOYO NA MISHIPA YA DAMU pamoja na BAADHI YA SARATANI, NA KIHARUSI.

Kuongezeka kwa mafuta mwilini husababisha ongezeko la uzito, hivyo kusababisha matatizo kamavile, MAUMIVU SUGU YA MGONGO,

 

MAUMIVU NA UHARIBIKAJI WA VIUNGO, pamoja na UCHOVU USIO NA SABABU.

Uwiano kati ya kiasi cha nishati lishe au nguvu (calories) tunazoingiza mwilini kwa kupitia chakula, na kiasi cha nishati lishe (calories) tunazotumia kwa kufanya mazoezi, ndiyo haswa kitu muhimu cha kuzingatia katika kuzuia ongezeko au kupunguza mafuta mwilini.

Mwili wako ukipata nishati lishe nyingi kuliko ile unayoitumia, kunakuwa na nishati lishe ya ziada mwilini. Nishati lishe au nguvu ya ziada hutunzwa mwilini kama MAFUTA. Na kama kila siku kunakuwa na nishati lishe ya ziada mwilini mwako, mafuta yataongezeka kila siku na utaongezeka uzito.

Kwa maana hiyo basi, tukila sana tunatakiwa tufanye mazoezi sana ili tuweze kuitumia nishati lishe yote tuliyoiingiza mwilini kwa kula sana. Tusipofanya hivyo, nishati lishe hii hutunzwa kama MAFUTA ndani ya miili yetu.

 

Haya hapa mambo matatu muhimu unayotakiwa kufahamu kuhusu kuudhibiti mwili wako:

 

  1. Ili kuzuia ongezeko la mafuta mwilini, tunatakiwa kuhakikisha kwamba tunatumia kiasi cha nishati lishe (calories), sawa na kile tunachoingiza mwilini. ( nishati lishe hutumika kwa kufanya shughuli za kila siku na mazoezi. Nishati lishe huingia mwilini kwa kula chakula, hususani vyakula vya WANGA na MAFUTA.

 

  1. Ili kupunguza kiasi cha mafuta mwilini, tunatakiwa kuhakikisha kwamba tunatumia kiasi cha nishati lishe (calories) zaidi ya kile tunachoingiza mwilini, hivyo kubaki na deni la nishati lishe (calorie deficit). Deni hili hulipwa kwa kutumia (kuchoma) mafuta mwilini kitu ambacho husaidia kupunguza mafuta na uzito.

 

  1. Kwa wale wanaotaka kuongezeka uzito kwa sababu maalumu, inatakiwa kuingiza mwilini kiasi kikubwa cha nishati lishe, zaidi ya kile kinachotumika. Kwa kufanya hivi kunakuwa na ziada ya nishati lishe (calorie excess) ambayo hutumika kuongeza mwili. Yako mambo muhimu ya kuzingatia ili kuhakikisha kuwepo kwa kuongezeka uzito kiafya. Kuongezeka uzito kiafya ni kuongezeka kwa misuli na siyo mafuta.

Fahamu kwamba, kwa ujumla miili yetu inatofautiana katika kutunza na kutumia nishati lishe (calories), kwa maana ya kwamba, twaweza kula aina na kiasi cha chakula kinachofanana, lakini tukatofautiana katika kuongezeka kwa mafuta mwilini. Kwa sababu hiyo hiyo, twaweza kufanya kiasi na aina ya mazoezi yanayofanana, lakini kukawa na tofauti katika kupungua kwa mafuta mwilini. Yapo mambo mengi yanayosababisha utofauti huu, ikiwa ni pamoja na umri, jinsia, kiasi cha misuli, ufanyaji kazi wa moyo pamoja na mambo mengine yanayohusishwa na vinasaba (urithishwaji).

hivyo basi, hakuna programu ya lishe au mazoezi inayoweza kufanya kazi kwa watu wote. kila mtu kutokana na uwezo wa mwili wake kutunza na kutumia nguvu inayoingia mwilini, anatakiwa kuwa na programu ya lishe na mazoezi inayoweza kufanya kazi kwa aina ya mwili wake”.

Bofya hapa kupakua muongozo wa lishe utakaokusaidia kupunguza mafuta na uzito, kuzuia kuongezeka kwa mafuta mwilini na kujikinga na magonjwa sugu, BILA KUATHIRI AFYA YAKO HATA KIDOGO.

Free Presentantion on ...

Free Presentation on Weight Loss with Zohra ...

+ View

Recent Articles

Utastaajabishwa na ...

Wakati mwingine tunakata tamaa kufanya mambo ...

+ View

Matatizo sugu yanayo ...

Wengi wetu tunafahamu umuhimu wa mazoezi katika ...

+ View

MEN’S BELLY FAT: Pride ...

The fact that abdominal fat, or belly fat, is not ...

+ View
  • Prev
  • Sponsor this Section
Scroll to top