Reputation Management
CPR certification onlineCPR certification online

 

Siku ya wafanyakazi duniani huadhimishwa tarehe 1 May kila mwaka, na nchi nyingi duniani zimeridhiria na kufanya maadhimisho haya kitaifa. Kwa mara ya kwanza sikukuu hii iliadhimishwa kimataifa mwaka 1891. Sehemu nyingi duniani sikukuu hii huambatana na maandamano ambapo wafanyakazi hukusanyika wakiwa na mabango yenye ujumbe na maoni maalumu kwa lengo la kuyawasilisha kwa waajiri.

Afya bora za wafanyakazi ni kiungo muhimu cha uzalishaji na utendaji bora. Waajiri wengi hawafahamu uhusiano uliopokati ya afya za wafanyakazi wao na uzalishaji na tija katika kazi. Japokuwa waajiri wote wanafahamu na wanakubaliana kuwa kuwekeza kwenye rasilimali watu kunaongeza ufanisi katika sehemu ya kazi, suala la madhara ya kiafya kwenye uzalishaji bado halijafanyiwa kazi kiasi cha kutosha. Uelewa wa umuhimu wa afya katika kazi umekuwa unaongezeka kutokana na msukumo wa sera na sharia mbalimbali zilizopelekea kuanzishwa kwa programu mbalimbali za kuwapatia wafanyakazi nafasi ya kupata elimu ya afya na hata fursa za kupimwa afya na kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao.

Kila mwajiri anawajibika kulinda afya za wafanyakazi wake, na hili huwa na tija kwa waajiri wengi wanaowajali watumishi wao. Kwa kuwa na programu bora za afya zinazotoa fursa ya matibabu kwa wafanyakazi na kuwa na mazingira salama ya kazi waajiri huwezi kuepuka gharama nyingi zinazotokana na madhara ya kiafya kazini.

Kutokuwa na programu bora za afya katika maeneo ya kazi huwagharimu kwa kiasi kikubwa waajiri, hasa pale wanapolazimika kupoteza siku za kufanya kazi pale wafanyakazi wanapokuwa wagonjwa. Pia watumishi wasio na afya bora hushindwa kufanya kazi kwa ufanisi hivyo kupunguza tija katika kazi zao. Ili wajiri waweze kupata wafanyakazi wenye tija ni muhimu kuwekeza katika afya zao. Ili kufanikisha lengo la kuwa na wafanyakazi wenye afya ni muhimu waajiri kuanzisha program za afya katika sehemu za kazi. Programu hizi zinashauriwa zilenge maeneo makuu mawili ambayo ni

1. Matibabu ya wafanyakazi 2. Kujikinga na magonjwa na kuhimiza mazoezi

Mambo yanayoweza kusaidia

• Programu za kiafya katika maeneo ya kazi, zinaweza kusaidia kuimarisha afya za wafanyakazi kwa kupunguza na kuzuia magonjwa yanayoweza kuathiri uzalishaji wa mfanyakazi. Hii itasaidia kupunguza gharama zinazotumika kwa matibabu ya magonjwa sugu yanayoweza kuzuiliwa na gharama za malipo kwa ulemavu au athari zitokanazo na kazi.

• Programu hizi pia humuimarisha mfanyakazi kiakili, na kisaikolojia kumuongezea stamina, uwezo wa akili kufanya kazi vizuri na kuongeza ufanisi kazini. Pia hii itapunguza hasara isiyo ya moja kwa moja kazini kama kutokuwepo kazini kutokana na kuumwa mara kwa mara na kuongeza uzalishaji.

Je nini gharama za kutokuwa na programu za afya kazini?

• Gharama za kutokutoa programu za afya kazini zinaweza kupimwa kwa kulinganishwa na

o Kutokuwepo kazini kutokana na ugonjwa au kuumia kazini

o Kupungua kwa malipo ya muda wa ziada ili kulipia nafasi iliyoshikiliwa na mtu mwingine wakati mfanyakazi anaposhindwa kufika kazini

o Gharama ya kuwekeza kwenye rasilimali watu ili kuwabadilisha wafanyakazi walio wagonjwa

Mpango mkakati wa afya katika sehemu ya kazi

Kati ya magonjwa yanayoongoza kwa gharama za matibabu na kupunguza ufanisi wa kazi ni magonjwa sugu mfano magonjwa ya moyo, magonjwa ya mifupa na misuli, kisukari n.k. Wafanyakazi wengi wanatumia muda wao mwingi wakiwa kazini kuliko sehemu nyingine. Kwa wastani wafanyakazi hutumia ya masaa 8-12 wakiwa kazini kwa siku tano za wiki. Hivyo waajiri wana nafasi ya kipekee ya kuhamasisha na kuboresha afya na usalama wa wafanyakazi na kuongeza uzalishaji kwa ujumla.

Kukiwa na programu za kiafya katika sehemu za kazi zinawezesha

• Kuleta mabadiliko katika mtazamo wa kijamii kuhusu afya na mazoezi

• Kuwezesha sera zinazohamasiaha afya makazini

• Kuongeza tabia zenye mwelekeo mzuri wa kiafya hasa katika chakula na tabia ya kufanya mazoezi

• Kuongeza uelewa wa wafanyakazi juu ya mambo ya kiafya

• Kusaidia wafanyakazi kufanya uchunguzi wa kiafya, chanjo zinazohitajika na kufuatilia matibabu

Program ya mpango wa afya kazini

Ili kuboresha afya ya wafanyakazi, waajiri wanaweza kuanzisha program za kiafya ambazo zinamsukumo kutoka kwa waajiriwa, na kuwapa mazingira mazuri na kuwaruhusu kujihusisha na programu mbali mbali za kiafya bila kuathiri utendaji wao wa kazi.

Mfano wa program za kiafya makazini ni kama

• Madarasa ya kuelimisha juu ya afya

• Kuwezeshwa kuhudhuria sehemu za mazoezi

• Sera zinazohamasisha afya katika mazingira ya kazi kama kuzuia uvutaji wa sigara

• Kuwa na bima ya afya kwa madhara yanayoweza kutokana na kazi husika na kwa ajili ya kupima afya

• Mazingira yaliyoboreshwa ya kufanyia kazi mfano kuwezesha vyakula vyenye kuimarisha afya kuwepo maeneo ya kazi au kantini za kazini

• Mazingira ya kazi yaliyoboreshwa kwa kuzuia madhara ya kiafya yanayoweza kujitokeza katika mahali husika, na kuwa na uwezo wa kutambua tatizo jipya linapojitokeza na kulifanyia kazi

Marejeo

1. Goetzel RZ, Hawkins K, Ozminkowski RJ, et al. The health and productivity cost burden of the ‘top-10_ physical and mental health conditions affecting six large US employers in 1999. J Occup Environ Med. 2003;45:5–14.

2. Partnership for Prevention. Leading by Example: CEOs on the business case for worksite health promotion. Washington, DC: 2005.

3. Stewart WF, Ricci JA, Chee E, Morganstein D. Lost productive work time costs from health conditions in the United States: results from the American productivity audit. J Occup Environ Med. 2003;45(12):1234-1246.

4. Finkelstein EA, Brown DS. Why does the private sector underinvest in obesity prevention and treatment? NC Med J. 2006;67(4): 310-312.

Nakala hii imeandaliwa kwa hisani ya tovuti ya CDC www.cdc.gov

 

Free Presentantion on ...

Free Presentation on Weight Loss with Zohra ...

+ View

Recent Articles

Utastaajabishwa na ...

Wakati mwingine tunakata tamaa kufanya mambo ...

+ View

Matatizo sugu yanayo ...

Wengi wetu tunafahamu umuhimu wa mazoezi katika ...

+ View

MEN’S BELLY FAT: Pride ...

The fact that abdominal fat, or belly fat, is not ...

+ View
  • Prev
  • Sponsor this Section
Scroll to top