Reputation Management
CPR certification onlineCPR certification online

Kwa kifupi: Katika Jamii zetu wako watu ambao mara nyingi tunakosea umri wao na kudhani wana umri mdogo kuliko wanavyoonekana. Wako pia ambao huonekana wenye umri mkubwa kuliko umri wao halisi. Japo wengi wanaweza kudhani kwamba mionekano hii hutokea tu kwa bahati, tafiti na uzoefu unaonyesha tofauti.

 

Kikubwa tunatakiwa kufahamu kwamba umri mkubwa si tatizo, tatizo ni madhara ya kiafya yanayoambatana na umri mkubwa. Madhara haya ndiyo huchangia kwa kiasi kikubwa katika kumfanya mtu aonekane tofauti.

Magonjwa na matatizo mengi kiafya hujitokeza zaidi pale umri unaposogea. Kuumwa mgongo, viungo na hata kushindwa kufanya au kufurahia tendo la ndoa ni miongoni mwa matatizo machache ambayo hujitokeza sana kadri umri unavyoongezeka. Matatizo haya huanza kujitokeza tunapofikisha umri wa miaka kati ya 25 na 30.

Ni matatizo haya na si vinginevyo, ndiyo huwatatiza watu wenye umri mkubwa.

“Hizi hapa tabia tano (5) za wanaume wasiotatizwa na umri mkubwa–ambazo katika hali ya kawaida umuhimu wake husahaulika.”

1. Hufanya mazoezi ya kunyanyua au kusukuma uzito

Mazoezi haya husaidia kudumisha misuli

Wengi wetu hupuuzia mazoezi ya aina hii kwa kusema ni mazoezi kwa ajili ya watunisha misuli na wenye kutaka kuwa na misuli mikubwa. La hasha, mazoezi haya ni muhimu katika kuzuia kupotea kwa nguvu na kiasi cha misuli–vitu ambavyo hutokea kadri umri unapokuwa ukiongezeka. Mazoezi haya pia husaidia kuzuia upungufu wa homoni ya kiume inayoitwa testosterone. Kiwango cha homoni hii mwilini hupungua kadri umri unavyoongezeka. Kupungua kwa kiwango cha homoni hii mwilini huchangia katika kusababisha tatizo la kupungukiwa kwa nguvu za kiume na kushindwa kufanya au kufurahia tendo la ndoa.

IGA TABIA HII: “Weka utaratibu wa kufanya mazoezi ya kunyanyua au kusukuma uzito angalau mara mbili au tatu kwa wiki. Kumbuka, kunyanyua au kusukuma uzito, haimaanishi kutumia uzito mkubwa utakaouzidi uwezo wako.”

2. Huendesha baiskeli

Kuendesha baiskeli ni mazoezi muhimu

Kuendesha baiskeli hukupa fursa ya kufanya mazoezi ya aina tofauti kwa wakati mmoja. Tafiti zimeonyesha kwamba watu wanaondesha baiskeli mara kwa mara hushi miaka mingi zaidi ya wale wanaotumia magari na pikipiki, na pia viungo na miili yao huwa na nguvu na uwezo wa kufanya kazi zaidi

DONDOO:

“Iga tabia hii kwa kuhakikisha unaendesha baiskeli kila unapopata fursa. Kama unaishi karibu na bara bara yenye sehemu maalumu iliyotengwa kwa ajili ya waendesha baiskeli, tumia fursa hiyo kuendesha baiskeli.”

3. Hufanya mazoezi ya kunyoosha na kulainisha viungo

Kunyoosha viungo ni muhimu kwa afya ya viungo

Kadri umri unavyoongezeka misuli na viungo huzidi kukakamaa. Hii inaweza kusababisha matatizo ya kushindwa kutembea vizuri, kuanguka na hata kuumia mara kwa mara. Mazoezi ya kujinyoosha hupunguza au kuzuia kukakamaa kwa misuli na viungo–hivyo kuzuia madhara yanayoweza kusababishwa na tatizo hilo

DONDOO:

”Iga tabia hii kwa kuhakikisha unafanya mazoezi ya kujinyoosha kabla au kila baada ya kufanya mazoezi. Kumbuka pia kujinyoosha mara kwa mara kama kazi yako inakufanya kuketi kwa muda mrefu.”

4. Hupata mapumziko ya kutosha

Mapumziko na kujumuika ni muhimu

Kazi na mambo mengi kama sehemu ya maisha, hutufanya tukose muda wa kupumzika ipasavyo. Kukosa mapumziko ya kutosha huifanya miili yetu kuchoka na hivyo kupoteza nguvu haraka pale umri unaposogea. Kutokupata mapumziko ya kutosha pia husababisha kuongezeka kwa vichocheo vya magonjwa mwilini na hata kupunguza kinga za miili yetu. Mapumziko ya kutosha husaidia kuzuia kupanda kwa kiwango cha homoni ya stress mwilini, hivyo kukufanya mwenye nguvu na furaha.

DONDOO:

“Iga tabia hii kwa kuhakikisha unapumzika kwa kupata usingizi wa kutosha (kulala kusikopungua masaa nanae kwa siku), kushiriki katika michezo na kujumuika na ndugu, jamaa na marafiki mara kwa mara.”

5. Hutumia virutubisho-lishe (nutritional supplements)

Umuhimu wa virutubisho-lishe huongezeka kadri umri unapoongezeka

Umri unapokwenda, uwezo wa miili yetu kutumia chakula tunachokula ipasavyo hupungua. Lakini pia uhitaji wa kula lishe bora huongezeka. Virutubisho lishe husaidia kuupa mwili uwezo wa kutumia chakula tunachokula na hata kuupa mwili virutubisho muhimu.

Ongea na daktari wako au mtaalamu wa lishe kuhusu uhitaji wa virutubisho-lishe. Daktari ataangalia hali yako na kukushauri kama unahitaji na hata kukushauri aina ya virutubisho-lishe unavyohitaji.

Free Presentantion on ...

Free Presentation on Weight Loss with Zohra ...

+ View

Recent Articles

Utastaajabishwa na ...

Wakati mwingine tunakata tamaa kufanya mambo ...

+ View

Matatizo sugu yanayo ...

Wengi wetu tunafahamu umuhimu wa mazoezi katika ...

+ View

MEN’S BELLY FAT: Pride ...

The fact that abdominal fat, or belly fat, is not ...

+ View
  • Prev
  • Sponsor this Section
Scroll to top