Reputation Management
CPR certification onlineCPR certification online

Utaratibu wa kuweka michoro mwilini (tattooing) na kujiweka vipini (piercing) ni utamaduni uliodumu kwa miaka mingi miongoni mwa jamii nyingi zikiwemo za kiafrika. Mifano mizuri ni wamakonde, Wagogo, wamasai na kadha wa kadha.

 Siku za usoni utaratibu huo umepata umaarufu hata kwa watu wanaotoka nchi zilizoendelea. Sababu mbali mbali zimepelekea Mabadiliko haya ambazo ni pamoja na swaga za mitindo ya kisasa, kuongeza mvuto, kuonyesha upeo wa kimapenzi, kuiga wengine hasa watu wanaotuvutia na kutuhamasisha (role models). Uamuzi wa kuweka mchoro au mapambo mengine mwilini ni uamuzi mkubwa unaoweza kubadili mtazamo wako kwa maisha na mtazamo wa wengine kwako, na pia unaweza kuwa na faida pia hasara au madhara. Kwa kuzingatia umuhimu wa hatua hii ni vizuri kufanya uamuzi kwa umakini hasa tunapoamua kuweka mapambo ya kudumu kwenye miili yetu. Mambo ya msingi ya kuzingatia ni pamoja na yafuatayo;

1. MCHORO NI WA KUDUMU AU WA MUDA MFUPI:

Kuna aina mbili ya michoro na vipini. Ya kwanza ni ile ya muda mfupi na nyingine ni ile ya kudumu. Ya muda mfupi huwa ni rangi za michoro zinazofutika na vipini vya kubandika ambavyo havisababishi mabadiliko kwenye mwili. Tofauti na hivi vya muda mfupi, michoro na vipini vya muda mrefu huwekwa mwilini na huwa sehemu ya mwili. Licha ya kwamba michoro na vipini hivi huweza kutolewa, utoaji wake huwa ni changamoto.

2. UNAWEKA MCHORO WA KITU GANI:

ni muhimu kuangalia aina ya mchoro unaouweka, lengo ni kuhakikisha mchoro unaoweka hauwezi kukuletea shida baadaye. Mfano kuweka mchoro au jina la mpenzi wako wa sasa ambaye mnaweza kuachana baadaye na ukapata usumbufu kuuondoa hasa unapopata mpenzi mwingine.

3. UNAWEKA MCHORO WAPI:

Je unapouweka mchoro unaweza kukuletea usumbufu baadaye? hili ni ni jambo la muhimu kuzingatia. Usumbufu waweza kuwa katika kazi yako baadaye, mahusiiano yako ya baadaye, biashara yako n.k. Vivyo hivyo mchoro pia unaweza pia kuboresha kazi yako au mahusiano yako.

4. ATHARI ZA KIAFYA ZA MICHORO NA VIPINI:

Kutoga na kuweka vipini mwilini

Ni vizuri kutambua uwekaji wa michoro na vipini unaweza kuambatana na matatizo mbali mbali ya kiafya:

a. Michoro (tattoo) 

- maambukizi ya virusi vya Ukimwi,

- homa ya manjano/ini,

- TB ya ngozi,

- maambukizi ya bakteria

- damu kuvilia kwenye ngozi (hematoma)

- kutoka damu nyingi

b. vipini (piercing)

- maambukizi kama hapo juu

- kupata makovu; hasa kwa watu wenye hulka ya kutoka makovu wanapopata majeraha.

- kuharibu meno, kuongea na kula kwa shida; kwa vipini vilivyo kinywani, hasa vinapogusana na meno.

- sumu ya vyuma vizito (heavy metal poisoning) kwa vipini vilivyotengenezwa na malighafi zenye madhara kwa mwili.

Hivyo ni muhimu mtumiaji kutambua vipini anavyotumia vimetengenezwa na nini.

5. NANI ANATOA HUDUMA:

hakikisha anayekupatia huduma ya mchoro au kukuwekea kipini ni mtaalamu wa hiyo kazi na anao uzoefu wa kutosha. a. Wapo watoa huduma wanaofanya kazi hii kwa kujifunza na hivyo kuhatarisha afya ya wanaohitaji huduma.

Watoa huduma wanatakiwa wajue jinsi ya kutunza ngozi ya mteja, kusafisha vifaa vya ktutolea huduma kwa namna inayoua vijidudu hatari na kuwa na utaalamu wa kupunguza utokaji wa damu na hata kudhibiti utokaji wa damu kama itatokea. Pia ni vizuri ajue jinsi ya kuuguza vidonda kama itatokea.

6. MAHALI HUDUMA ZINAPOTOLEWA:

hakikisha mahali huduma inapotolewa ni salama na vifaa vinavyotumika ni salama. Viwe vinasafishwa kwa kuchemshwa kwa joto linalostahili kuua virusi na bakteria. Na hakikisha vifaa vya kukutoboa havitumiki kwa mtu zaidi ya mmoja. Pia ni vizuri kujiridhisha kuwa mazingira ya utoaji huduma yanakufanya uwe na amani na utulivu wa kupata huduma unayostahili.

7. KUUCHOKA AU KUUKINAI MCHORO AU KIPINI:

baadhi ya watu wanaweza kuhisi kuuchukia au kuuchoka mchoro. Hivyo ni vizuri kujiridhisha na aina ya mchoro au kipini unachoweka. Inapotokea hali ya kuuchoka mchoro au kipini inaweza kuleta usumbufu na wakati mwingine inaweza kusababisha sonona (depression). Hili hutokea zaidi pale uamuzi wa kuweka mchoro au kipini unapofanyika haraka bila tafakari ya kutosha

8. GHARAMA ZA KUONDOA MICHORO NA VIPINI:

Uondoaji wa michoro ya kudumu mara nyingi huhitaji upasuaji, ambao unaweza kugharimu muda, pesa na kusababisha maumivu. Kuondoa vipini ni rahisi kwa kuwa unavitoa pale vilipowekwa. pamoja na urahisi huu mahali hapo hubaki na tundu au nafasi iliyotengenezwa kwa ajili ya kipini hicho.

9. TAFUTA USHAURI:

Omba ushauri kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki kabla ya kuamua kuweka mchoro mwilini au kipini. Chukua muda wa kutosha kutafakari juu ya uamuzi wako.

10. USHAURI WA KITAALAMU:

Tafuta ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya ili kuweza kuepuka athari za kiafya unazoweza kupata kutokana na michoro au kuweka kipini mwilini. Ushauri wa afya unaweza kuupata kwa kuongea na wataalamu wa afya moja kwa moja au kusoma hasa katika vyanzo vya kuaminika vya habari za afya.

HITIMISHO

Michoro na vipini vinawekwa mwilini kwa lengo la kukufanya uufurahie mwonekano wako na kukufanya ujisikie vizuri. Kuzingatia mambo yaliyotajwa hapo juu kutakusaidia kufanya uamuzi ulio sahihi utakaokufanya ufikie lengo lako la kuboresha muenokano na si kukultea huzuni na kujilaumu.

Free Presentantion on ...

Free Presentation on Weight Loss with Zohra ...

+ View

Recent Articles

Utastaajabishwa na ...

Wakati mwingine tunakata tamaa kufanya mambo ...

+ View

Matatizo sugu yanayo ...

Wengi wetu tunafahamu umuhimu wa mazoezi katika ...

+ View

MEN’S BELLY FAT: Pride ...

The fact that abdominal fat, or belly fat, is not ...

+ View
  • Prev
  • Sponsor this Section
Scroll to top