Reputation Management
CPR certification onlineCPR certification online

NIA NI KUPUNGUZA UZITO AU MAFUTA, NA SIYO KUKONDA MWILI

KWA UFUPI: Jamii ya wa Tanzania kwa sasa inao muamko mkubwa sana katika swala zima la kupambana na unene uliokithiri. Watu wanajituma kwa nia na haja. Sababu za kupambana na janga hili la uzito au unene uliokithiri ziko nyingi. Kuna wanaotaka kuwa na muonekano mzuri, kupendeza wanapovaa magauni au nguo zao za harusi, na wengine wana nia ya kujikinga na magonjwa sugu.

 

 

 

Kwa ujumla swala la kupambana na unene uliokithiri ni jambo zuri, iwe ni kwa nia ya kuwa na muonekano mzuri au kujikinga na magonjwa. LAKINI KATIKA ZOEZI HILI, KUNA TATIZO MOJA KUBWA. Watu kushindwa kutofautisha kati ya kupunguza uzito na kukonda.

 

Kuna tatizo pia katika kutofautisha vitu viwili: KUFANYA "DIET" NA KUJIKONDESHA 

 

UZOEFU: Asilimia kubwa ya watu hususani kina dada na wanawake, hupambana na tatizo hili la unene kwa kufanya kile wanachokiita "diet". Mtaani ziko diets chungu nzima, na kiukweli ni vigumu kuthibitisha kama zinatolewa na watu wenye taaluma na weledi, au ni tatizo lile lile, linalotukumba wengi-tatizo la kukamata fursa na kufaidika na ile dhana ya watu kupenda SHORT CUTS.

 

Uzoefu ni kwamba, ukizifuatilia diets nyingi wanazozitumia watu, huchelewi kugundua makosa chungu nzima. Mara nyingi diets hizi zinakuwa hazijitoshelezi, hivyo kunfanya anayetumia kukosa virutubisho muhimu sana mwilini.

Ukifuatilia diets hizo kwa umakini, hakuna muujiza, ni lazima uta pungua, tena ndani ya muda mfupi sana. Lakini, kiuhalisia kinachotokea si kupungua uzito au unene, bali ni KUKONDA MWILI NA KUDHOOFU. 

 

Mfano diet inayomlazimu mtu kutokutumia kabisa, au kutumia kiasi kidogo sana cha vyakula vya WANGA. Kibaiolojia, mojawapo ya mambo yanayofanywa na wanga ni kusaidia chembe hai au seli za mwili kutunza maji. Unapokosa kiasi cha wanga ambao kwa kawaida unahitajika, chembe hai zako hazitaweza kutunza maji, baadala yake zitapoteza maji. Kwa maana hiyo mwili wako utapoteza maji. Kutokana na kupoteza maji, chembe hai za mwili pamoja na mwili wote, vitasinyaa. Kutokana na kusinyaa mtu hujiona amepungua, wakati kilichotokea ni kupoteza maji, kitu ambacho si kizuri kiafya. Kupungua huku huambatana na kudhoofu, kutokupendeza na kuonekana kuchoka. Kiukweli, si kitu kizuri kiafya. 

 

Mfano mwingine ni diet inayomlazimu mtu kula chakula kidogo sana. Unakuta wengine wanakula mboga mboga na matunda na kiasi kidogo sana cha protini. Kwa kuwa chakula hicho kinakuwa kidogo sana, virutubisho vya kuupa mwili nguvu vinakuwa havitoshi, hivyo mwili unakosa nguvu unayohitaji. Virutubisho vya kujenga mwili au protini vinakuwa pia havitoshi. Kukosekana kwa protini na nguvu ya kutosha kunasababisha mwili kutumia misuli kutengeneza nguvu. Hii inasababisha kupoteza chembe hai za misuli na mwisho wa siku kupoteza kiasi cha misuli. Mwili ukipoteza misuli ambayo katika hali ya kawaida inahitajika, kinachokuwa kimetokea SI KUPUNGUA, bali ni KUKONDA. 

 

"Ikumbukwe kwamba, nia na madhumuni ya kupunguza uzito au unene, ni kupunguza kiasi cha mafuta yaliyozidi mwilini na wala si kupunguza misuli. Hivyo basi program yeyote inayolenga kupunguza uzito/unene, lazima izingatie kutunza misuli ya mwili"

 

Kwa kifupi kinachotokea ni watu kujinyima chakula na kujichosha. Kwa maana halisi zoezi la kufanya diet au dieting linakuwa limebadilika na kuwa-KUSHINDA NJAA. Kwa lugha ya kiingereza kinachokuwa kimetokea ni STARVING na siyo DIETING. 

 

Matokeo ya haya yote ni KUKONDA, wala siyo KUPUNGUA. Maana yake ni kwamba, mtu anakuwa amepunguza kila kitu ikiwa ni pamoja na misuli na maji-vitu ambavyo havitakiwi kupungua mwilini. Kuna kuwepo pia na ukosefu wa madini na vitamin muhimu kutokana na ukweli kwamba baadhi ya diets hizi zinamfanya mtu kuacha kula vyakula ambavyo ni muhimu, lakini pia zinamlazimu mtu kula chakula kidogo zaidi ya mwili wake unavyohitaji. 

 

Haya yote humfanya mtu kudhoofu, kutokuwa na nguvu, kuonekana amechoka na ngozi kutokuwa na nuru yake ya asili.  

Kutokana na kudhoofu na kukosa nguvu, watu wengi hushindwa kuendelea na program zao za kupunguza uzito, hivyo kujikuta wanarudia kule kule-kula hovyo na kuongezeka uzito mara dufu.

 

HITIMISHO: Hakikisha unaelewa tofauti kati ya kupungua uzito/unene na kukonda. Pia ni vyema kuelewa tofauti kati ya kufanya diet (DIETING) na kushinda au kubaki njaa (STARVING). Kiafya, tunawashauri watu kupunguza uzito/unene na tunapinga KUKONDA.  

 

Fanya programu ambayo itakuwa ni sehemu ya maisha yako, maana kupunguza uzito ni SAFARI na wala si MAHALI useme utasafiri kwa kutumia chochote ili mradi ufike haraka. Hii ni safari ambayo unakuwa safarini katika siku zote za maisha yako. Hivyo chagua programu ambayo haikuchoshi, haikuletei shida ya bajeti na unayoifanya kwa furaha.

 

Hakikisha unafahamu kazi na madhara ya kila unachokifanya katika mwili wako. Usikubali kutumia kitu bila kuwa na sababu yakinifu. Mfano mtu anakuambia asubuhi kula tango moja na maziwa ya mtindi peke yake. Ufahamu kabisa kwa kufanya hivyo unakuwa umeunyima mwili nguvu ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya shughuli unazokwenda kufanya katika siku hiyo. Hivyo basi si muujiza wewe kujisikia umechoka na hata kusinzia ovyo ukiwa kazini.

Free Presentantion on ...

Free Presentation on Weight Loss with Zohra ...

+ View

Recent Articles

Utastaajabishwa na ...

Wakati mwingine tunakata tamaa kufanya mambo ...

+ View

Matatizo sugu yanayo ...

Wengi wetu tunafahamu umuhimu wa mazoezi katika ...

+ View

MEN’S BELLY FAT: Pride ...

The fact that abdominal fat, or belly fat, is not ...

+ View
  • Prev
  • Sponsor this Section
Scroll to top