Reputation Management
CPR certification onlineCPR certification online

 MAANA: Watoto wadogo hukojoa bila kuweza kujizuia mpaka wanapofikisha umri wa miaka mitano. Katika umri huu watoto huacha kukojoa kitandani na huwa na uwezo wa kuamka na kwenda chooni. Iwapo mtoto aliyefikisha umri wa miaka mitano anaendelea kukojoa kitandani hili huchukuliwa kama tatizo, ingawa wapo watoto wanaoweza kuendelea kukojoa kitandani mpaka wanafikisha umri wa miaka 7-8. Kimsingi kukojoa kitandani ni tatizo kama mtoto ataendelea kukojoa kitandani baada ya kufikisha miaka 5 (wengine miaka 7-8), au anaanza kukojoa kitandani baada ya kuwa alishaacha kufanya hivyo.

 Kuna aina mbili ya tatizo hili la kukojoa kitandani:

1) watoto ambao hawajawahi kuacha kukojoa kitandani (kitaalamu inaitwa primary enuresis )

2) watoto waliokwisha kuacha kukojoa kitandani ambao wanaanza kukojoa kitandani tena (kitaalamu secondary aneuresis).

UKUBWA WA TATIZO: Inakadiriwa kuwa asilimia 15% ya watoto wenye umri wa miaka zaidi ya 5 wana tatizo la kukojoa kitandani.

SABABU ZA KUKOJOA KITANDANI: kukojoa kitandani ni tatizo la kiafya na siyo uamuzi wa mtoto. Pia inaweza kuwa sehemu ya ukuaji wa mfumo wa fahamu unaosimamia njia ya mkojo–kwa baadhi ya watoto mfumo huu huchelewa kukua. Hii ndiyo sababu baadhi ya watoto huacha kukojoa baada ya kufikisha miaka 7-8.

Kuna sababu kadhaa zinazoweza kusababisha tatizo hili. Baadhi ya sababu hizo ni;

 • Kuwa na utengenezaji wa mkojo kwa kiwango kikubwa wakati wa usiku (nocturnal polyuria)

 • Kuwa na kibofu cha mkojo chenye uwezo mdogo wa kutunza mkojo ( decreased bladder capacity)

 • Misuli ya kibofu kufanya kazi kwa nguvu zaidi (detrusor over activity)

 • Tatizo la kuamka usiku (sleep arousal disturbances)

 • Shida ya mawasiliano kati ya kibofu na ubongo (bladder brain connection dysfunction)

 • Kuchelewa kukua kwa ubongo (global maturation delay)

 • Pia zipo sababu nyingine mbali mbali ambazo daktari anaweza kuzitambua kulingana na dalili alizo nazo mtoto na vipimo vitakavyoonyesha zikiwa ni pamoja na;

  • Kurithi vinasaba vya hilo tatizo, wazazi wa watoto wenye matatizo ya kukojoa kitandani nao wanaweza kuwa walikuwa na tatizo hilo wakiwa watoto.

  • Kuwa na tatizo la maambukizi ya bakteria kwenye kibofu cha mkojo (UTI)

  • Kupata choo mara chache sana na choo kuwa kigumu (constipation)

NINI MZAZI ANATAKIWA AFANYE: Wazazi wenye mtoto mwenye tatizo la kukojoa kitandani wanatakiwa wazingatie yafuatayo;

 • Watambue mtoto wao ana tatizo la kiafya

 • Kutomuadhibu mtoto kwa sababu hajaamua kuwa na tatizo la kukojoa kitandani

 • Kumpenda mtoto na kuongea naye kwa lugha nzuri, na kujitahidi kumpa moyo kuwa hilo ni tatizo la kiafya

 • Kuacha kumsema kwa watu wengine na hasa kwa watoto wenzie kwa kuwa hiyo itamuathiri kisaikolojia

 • Kumpongeza kwa kila siku anayokuwa hakukojoa kitandani, ikiwezekana kumpatia zawadi ya namna fulani.

 • Kumpeleka hospitali ili apatiwe uchunguzi na kupatiwa tiba

 • Pia watambue tiba ya tatizo hili inachukua muda mrefu wakati mwingine na inahitaji uvumilivu kwa upande wa wazazi.

Watoto wenye tatizo la kukojoa kitandani wanatakiwa wapelekwe kwa daktari wa watoto na pia daktari wa magonjwa ya figo ya watoto.

Free Presentantion on ...

Free Presentation on Weight Loss with Zohra ...

+ View

Recent Articles

Utastaajabishwa na ...

Wakati mwingine tunakata tamaa kufanya mambo ...

+ View

Matatizo sugu yanayo ...

Wengi wetu tunafahamu umuhimu wa mazoezi katika ...

+ View

MEN’S BELLY FAT: Pride ...

The fact that abdominal fat, or belly fat, is not ...

+ View
 • Prev
 • Sponsor this Section
Scroll to top