Reputation Management
CPR certification onlineCPR certification online

Si kitu cha ajabu kukuta wazazi wakiwakataza watoto wao kushiriki katika michezo, kutokana na kile wanachoamini kwamba, mtoto kushiriki katika michezo ni kupoteza muda wa masomo. Ni ukweli pia kwamba kumekuwa na tabia ya shule nyingi kupunguza muda wa vipindi vya michezo ili kuwapa wanafunzi muda mwingi zaidi wa kukaa darasani. 

Wakati haya yote humnyima mtoto fursa ya kufanya mazoezi na hivyo kumuongezea uwezakano wa kupata magonjwa sugu kama kisukari, saratani na magonjwa ya moyo. Lakini ikumbukwe pia kwamba, kumpunguzia mtoto muda wa kufanya mazoezi huenda kukawa hakumuongezei uwezo wa kufikiri, wala kumfanya kuwa mwenye kumbukumbu bora. 

Hapa tunajadili umhimu wa mazoezi na michezo katika kumfanya mtoto awe na utashi darasani

1. MAZOEZI NA MICHEZO HUSAIDIA KATIKA KUBORESHA KUMBUKUMBU NA TABIA

Furaha ya mtoto ni michezo

Tafiti zinaonyesha kwamba kushiriki katika michezo na mazoezi mara kwa mara huwasaidia vijana na watoto kufikiri vizuri, kuwa na kumbu kumbu na kuwa na tabia nzuri kwa ujumla. Hii inatokana na uwezo wa mazoezi kuongeza vichocheo muhimu mwilini ambavyo huboresha kumbu kumbu ya mtoto.

2. MICHEZO HUONGEZA UWEZO WA KUSOMA NA KUFANYA HESABU

Ziko shahidi na sababu za kisayansi zinazoonyesha umuhimu wa michezo kwa watoto

Tofauti na watu wengi wanavyodhani, matokeo ya tafiti yanaonyesha kwamba wanafunzi wanaoshiriki zaidi katika michezo, ndiyo hufaulu zaidi somo la hisabati. Katika mojawapo ya tafiti hizi ilibainika kwamba wasichana waliohudhuria zaidi vipindi vya michezo shuleni, ndiyo waliopata maksi za juu zaidi katika somo la hisabati ukilinganisha na wale wasioshiriki kabisa.

3. VIPINDI VYA MICHEZO HAVIMPOTEZEI MTOTO MUDA WA MASOMO

Michezo ni kichocheo muhimu kwa utashi wa mtoto

Kutokana na tafiti, hakuna kutumia muda wa michezo kusoma, hakumuongezei mtoto uwezo na ufaulu katika mitihani yake. Tafiti hizi zinaonyesha kwamba, akili ya mtoto huchangamshwa na vipindi vya mara kwa mara vya michezo, na kutokumpa mtoto fursa ya kufanya hivyo ni kuichosha akili yake.

5. MICHEZO HUMPA MTOTO FURSA YA KUJUMUIKA

Kujumuika ni fursa muhimu sana kwa ukuaji na akili ya mtoto

Watoto wenye ratiba za michezo hupata fursa ya kujumuika na wenzao kitu ambacho huwasaidia kujikinga na maradhi ya akili. Watoto wasiojumuika mara kwa mara huweza kukumbwa na maradhi ya akili hapo baadaye. Kutokana na tafiti watoto hawa huwa na matatizo madogo madogo ya akili (personality problems), ambayo wazazi wao hushindwa kuyatambua mapema. Matatizo hayo yakiwa sugu huweza kuwa maradhi makubwa ya akili kama sonono (depression) na maradhi mengine kama hayo.

 USHAURI UNAOTOKANA NA USHAHIDI WA KISAYANSI 


Ushauri wa shirika la afya duniani (WHO)

Kutokana na shirika la afya duniani watoto na vijana wenye umri chini ya miaka kumi na nane (18) wanatakiwakutimiza angalau lisaa limoja (dakika sitini) la mazoezi ya kiwango cha kati na cha juu kwa siku. Kwa kufanya hivyo watoto hujikinga na maradhi sugu yasiyo ambukizi kama vile kisukari, magonjwa ya moyo na baadhi ya saratani. Maradhi haya huweza kuja kuwapata baadaye, au hata kuanza katika umri mdogo sana.

Kwa maana hiyo ni vema kwa wazazi na waalimu kuzingatia michezo kwa wanafunzi kama sehemu ya afya ya mtoto, na kuondokana na dhana potofu ya kudhani mazoezi humpotezea mtoto muda.

Free Presentantion on ...

Free Presentation on Weight Loss with Zohra ...

+ View

Recent Articles

Utastaajabishwa na ...

Wakati mwingine tunakata tamaa kufanya mambo ...

+ View

Matatizo sugu yanayo ...

Wengi wetu tunafahamu umuhimu wa mazoezi katika ...

+ View

MEN’S BELLY FAT: Pride ...

The fact that abdominal fat, or belly fat, is not ...

+ View
  • Prev
  • Sponsor this Section
Scroll to top