Reputation Management
CPR certification onlineCPR certification online

Kwa nini mazoezi ni muhimu katika kuzuia na kuudhibiti ugonjwa wa kisukari?

Jumatatu ya tarehe 14 Novemba ilikuwa ni siku ya KISUKARI duniani. Ujumbe wa mwaka huu ulikuwa ukisisitiza macho yote kuelekezwa katika kuutizama ugonjwa huu unaonekana kuongezeka kwa kasi sana katika Jamii ya waTanzania. Kikubwa kilichosisitizwa ni umuhimu wa kupima ili kuweza kuchukua hatua madhubuti mapema.

Wengi wetu tayari tunafahamu ukweli kwamba kutokufanya mazoezi kunachangia kwa kiasi kikubwa sana katika kusababisha ugonjwa huu. Lakini huenda bado haijatuingia akilini ni jinsi gani mazoezi huweza kusaidia katika kuzuia na hata kudhibiti sukari kupanda kwa watu ambao tayari wana ugonjwa wa kisukari.

Leo tutajadili sababu kubwa tatu zinazofanya mazoezi kuwa moja wapo ya tiba na kinga ya ugonjwa wa kisukari.

MAZOEZI HUSAIDIA KUPUNGUZA MAFUTA MWILINI

Mazoezi ya aerobics au cardio husaidia kupunguza mafuta mwilini

Moja wapo ya vitu vinvyochangia katika kusababisha ugonjwa wa kisukari aina ya pili (type 2 diabetes) ni ongezeko la mafuta mwilini. Mafuta yanapoongezeka mwilini huzifanya chembe hai za misuli kushindwa kutumia homoni ya insulin vizuri. Homoni ya insulin ndiyo kichocheo muhimu kinachosaidia sukari kuweza kutumika kutengeneza nguvu mwilini. Kushindwa kwa misuli na viungo vingine kuitumia homoni hii, husababisha sukari kubaki kwenye damu hivyo kuongezeka na kusababisha kisukari au kuleta madhara kwa wale ambao tayari wana ugonjwa huo.

Kufanya mazoezi husaidia kupunguza mafuta mwilini hivyo kuifanya homoni ya insulin kufanya kazi kwa ufanisi. Kwa kufanya hivyo sukari huweza kutumika ipasavyo katika kutengeneza nguvu mwilini. Kwa maana hiyo inakuwa haibaki katika damu.

MAZOEZI HUSAIDIA MISULI KUTUMIA SUKARI

Mazoezi kama mbadala wa kutumia sukari mwilini

Katika hali ya kawaida, asilimia zaidi ya 70 ya sukari inayopatikana katika chakula hupelekwa katika misuli (skeletal muscle) mara tu baada ya mlo. Hii ina maana kwamba ufanyaji kazi wa misuli ni muhimu sana katika kuifanya sukari itumike mwilini. Misuli huweza kutumia sukari kwa kupitia njia mbili tofauti. Ile inayohitaji insulin (insulin dependent pathway) na ile isiyohitaji insulin ambayo husababishwa na mazoezi (non-insulin dependent pathway). Kwa mgonjwa wa kisukari, kutokana na ukweli kwamba insulin haifanyi kazi vizuri, ina maana kwamba kutumia sukari kwa njia inayotegemea insulin hakufanyi kazi. Kwa maana hiyo basi, njia pekee inayokuwa imebaki ni ile ya kutumia mazoezi.

Kwa lugha rahisi ni kwamba, wakati njia ya kutumia sukari kwa kutegemea insulin haifanyi kazi kwa mgonjwa wa kisukari, njia inayosababishwa na mazoezi huwa njia mbadala inayouwezesha mwili wa mtu mwenye kisukari kuweza kutumia sukari, licha ya insulin yake kutokufanya kazi vizuri.

Kwa maana hiyo kufanya mazoezi ni muhimu sana kwa mgonjwa wa kisukari aina ya pili (type 2 diabetes) maana hii humpa fursa ya mwili wake kuweza kuitumia sukari inayotoka katika chakula, hivyo kuzuia isiongezeke katika damu.

MAZOEZI HUSAIDIA KUONDOA MSONGO WA MAWAZO

Mazoezi hushusha kiwango cha vichocheo vya msongo wa mawazo

Tafiti zinaonyesha kwamba msongo wa mawazo wa kupitiliza huweza pia kuchangia katika kusababisha magonjwa sugu kama kisukari. Hii inatokana na ukweli kwamba msongo wa mawazo au stress husababisha ongezeko la muda mrefu la homoni inayoitwa cortisol. Homoni hii hujuliakana kama homoni ya msongo wa mawazo (stress hormone).

Kuongezeka kwa kichocheo cha msongo wa mawazo (cortisol) kwa muda mfupi ni muhimu, kwani hutusaidia kuweza kufanya kazi na kutimiza majukumu. Bila stress kidogo tusingeweza kutimiza majukumu.

Tatizo ni pale homoni hii inapokuwa imeongezeka kwa muda mrefu. Kuongezeka huku kwa muda mrefu husababisha homoni ya insulin kutokufanya kazi ipasavyo (insulin resistance) kitu ambacho husababisha ugonjwa wa kisukari aina ya pili. Mazoezi ya mara kwa mara husaidia kuzuia kuongezeka kwa muda mrefu kwa homoni ya cortisol, kitu ambacho huifanya homoni ya insulin kufanya kazi vizuri. Homoni ya insulin inapofanya kazi vizuri sukari hutumika ipasavyo hivyo kutokuongezeka katika damu.

HITIMISHO

Mazoezi ni zaidi ya kupunguza mafuta na kuzuia unene. Hakikisha unajenga tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara bila kujali kama wewe ni mnene au mwembamba.

Free Presentantion on ...

Free Presentation on Weight Loss with Zohra ...

+ View

Recent Articles

Utastaajabishwa na ...

Wakati mwingine tunakata tamaa kufanya mambo ...

+ View

Matatizo sugu yanayo ...

Wengi wetu tunafahamu umuhimu wa mazoezi katika ...

+ View

MEN’S BELLY FAT: Pride ...

The fact that abdominal fat, or belly fat, is not ...

+ View
  • Prev
  • Sponsor this Section
Scroll to top