Reputation Management
CPR certification onlineCPR certification online

 

    

picha hizi zinaonyesha kabla ya matibabu ya mapengo

    

picha hizi zinaonyesha baada ya matibabu ya mapengo

Imehaririwa na Dr Lorna Carneiro D.D.S., PhD., (Mhadhiri MUHAS na Daktari Bingwa wa Meno bandia - Prosthodontists)

Mapengo ni tatizo linalotokana na kupoteza jino moja au zaidi. Mapengo hasa meno ya mbele, hupunguza kujiamini na huweza kumfanya mtu kuwa na aibu mbele za watu, au kumfanya asipende kujichanganya kwenye shughuli zinazohusisha watu wengi. Pamoja na kuichukia hali hii, kuna wengine hawafahamu kama mapengo yanaweza kutibiwa. Binadamu huwa ana aina mbili za meno, ya utotoni na a ukubwani.

Read more ...

Imehaririwa na Dr E.G.S Mumghamba D.D.S., MDent., Ph.D. (Muhadhiri MUHAS na Daktari Bingwa wa magonjwa ya fizi-Periodontologist)

Tatizo la kunuka kinywa, huwasibu watu wengi, na huwa kero kubwa kwa waliokaribu na mwenye tatizo hili. Mara nyingi mwenye tatizo hili huwa hafahamu, na wengi huona vibaya kumweleza mtu mwingine kuwa kinywa chake kinatoa harufu. Na wenye tatizo hili pia wakifahamu hupata mfadhaiko sana wa mawazo, na kutopenda kuongea kwenye kusanyiko la watu kwa kuhofia kuwakera wanaomsikiliza. Tatizo hili linaweza kupatiwa ufumbuzi iwapo mwenye tatizo atafahamishwa na hivyo kutafuta tiba stahiki.

Read more ...

 

Picha inaonyesha tatizo la meno kahawia [picha kwa hisani ya Dr Roman Francis]

Fluorosis ni mvurugiko maalum katika mchakato wa utengenezwaji wa sehemu ngumu za meno (enamel). Mvurugiko huu husababisha mabadiliko katika muonekano, uimara na ubora wa meno yaliyoathirika. Fluorosis hutokea pale ambapo madini ya floraidi mengi kupita kiasi yanapojumuishwa kwenye meno wakati yanapokuwa yanatengenezwa mwilini. Kiwango cha floraidi kinachokubalika mwilini kwa afya kwa siku ni 0.05mg mpaka 0.07 mg F/Kg/day. Madhara na ukubwa wa tatizo la fluorosis una uhusiano wa moja kwa moja na jumla ya kiwango cha madini ya floraidi yaliyokuwa mwilini wakati wa kipindi cha utengenezwaji wa meno.

Read more ...

 

1. Kutafuna kucha

Tabia hii inaweza kusababisha sehemu ya jino kusagika, kuwa dhaifu na hata kuvunjika. Pia na matatizo katika viungo vya taya na hivyo kuleta maumivu karibu na eneo la masikio (Temporomandibular joint dysfunction). Chanzo cha tabia hii chaweza kuwa ni mazoea tu, au msongo wa mawazo, kazi, n.k. Ili kuacha tabia hii kata kucha kwa kutumia kifaa maalumu kwa wakati, epuka msongo wa mawazo, kuwa na mpangilio mzuri wa kazi zako.

Read more ...

Free Presentantion on ...

Free Presentation on Weight Loss with Zohra ...

+ View

Recent Articles

Utastaajabishwa na ...

Wakati mwingine tunakata tamaa kufanya mambo ...

+ View

Matatizo sugu yanayo ...

Wengi wetu tunafahamu umuhimu wa mazoezi katika ...

+ View

MEN’S BELLY FAT: Pride ...

The fact that abdominal fat, or belly fat, is not ...

+ View
  • Prev
  • Sponsor this Section
Scroll to top