Reputation Management
CPR certification onlineCPR certification online

Afya ya kinywa ni muhimu kwa ajili ya afya ya mwili wako. Kuweka miadi na kwenda kumwona daktari wa afya ya kinywa ni muhimu sana, itakuwezesha kugundua matatizo ya afya ya kinywa mapema, ambapo matibabu yake huwa rahisi na yasiyo na gharama kubwa. Kupata uchunguzi wa daktari wa afya ya kinywa unakuwezesha kugundua baadhi ya magonjwa ambayo dalili zake za mwanzo huweza kutokea mdomoni.

Hizi hapa ni dalili 15 zinazoashiria unahitaji kumwona daktari wa afya ya kinywa

• Meno yako kuwa na ukakasi yanapokutana na vitu vya baridi au vya moto

• Fizi zako zimevimba pamoja na /au zinatoa damu ukisafisha kinywa kwa mswaki au uzi maalumu wa kusafisha katikati ya meno

• Una meno yaliyozibwa/kujazwa, au yamewekewa kofia maalumu ya meno (crown), kinywani una vipandikizi (dental implants) au una meno ya bandia

• Hupendi mwonekano wa meno yako/unaona shida kutabasamu mbele za watu

• Mdomo wako unatoa harufu mbaya au unahisi ladha mbaya mdomoni

• Umekuwa mjamzito

• Una maumivu, au uvimbe mdomoni au hata usoni

• Unapata shida ya kutafuna kutokana na maumivu au shida ya kumeza chakula

• Katika familia yako kuna historia ya matatizo ya fizi na meno

• Kama una tatizo lolote sugu la kiafya kama ugonjwa wa kisukari, ugonjwa wa moyo, ugonjwa wa ukimwi,

• Kama mdomo wako huwa mate yanakauka mdomoni mara kwa mara

• Unavuta sigara au matumizi yoyote ya tumbaku

• Unapatiwa matibabu kama ya mionzi, au unatumia madawa ya saratani au unapatiwa matibabu ya vichocheo (hormone replacement therapy)

• Mdomo wako unagoma na unauma wakati wa kufungua na kufunga au ukitafuna au unapoamka asubuhi, na meno hayakutani vizuri

• Una uvimbe usio na dalili zozote mdomoni na hauna dalili ya kupungua

Uonapo dalili hizo hapo juu nenda kwa daktari wa afya ya kinywa kwa ushauri na matibabu. Unashauriwa kwenda kwa daktari wa afya ya kinywa na meno angalau mara moja kwa mwaka hata kama huna dalili zozote zilizotajwa hapo juu.

Free Presentantion on ...

Free Presentation on Weight Loss with Zohra ...

+ View

Recent Articles

MEN’S BELLY FAT: Pride ...

The fact that abdominal fat, or belly fat, is not ...

+ View

Kuondoa kitambi, tumia ...

Nadhani katika kitu ambacho wengi wanapambana ...

+ View

Ushauri wa mazoezi kwa ...

Ni kawaida kwa watu wenye umri wa miaka 50 na ...

+ View
  • Prev
  • Sponsor this Section
Scroll to top