Reputation Management
CPR certification onlineCPR certification online

 

Kusafisha kinywa kwa usahihi kunahusisha matumizi ya

1. Mswaki

2. Uzi wa kusafisha kati ya meno (dental floss)

3. Vijiti vya kuchokonoa kati ya meno

1. KUPIGA MSWAKI

Muda sahihi wa kupiga mswaki

Inashauriwa usipige mswaki ndani ya muda wa dakika thelathini mara baada ya kula au kunywa.

 “Tafiti zimeonyesha kuwa na uwezekano wa enameli kulainika na kumomonyoka pale inapokutana na vyakula au vinywaji vyenye tindikali. Kupiga mswaki mara       baada ya kutumia vyakula au vinywaji vyenye tindikali huongeza uwezekano wa kuondoa sehemu ya enameli iliyolainishwa na vitu hivyo. Matumizi ya maji ya kunywa au kusukutua mara baada ya kula inapunguza uwezekano wa enameli kumomonyoka. Muda wa dakika thelathini toka kumaliza kula au kunywa, sehemu ya enameli iliyolainika huwa inakuwa imeimarika hivyo kupunguza uwezekano wa kuondolewa na mzunguko wa mswaki”

Piga mswaki mara mbili kwa siku kwa muda wa dakika mbili, kutakuwezesha kuondoa mabaki ya chakula na kuondoa ugavu ambao unaweza kudhuru meno na ufizi.

Kupiga mswaki kwa kufuata mpangilio maalumu (systematic toothbrushing)

Weka brashi za mswaki kwenye meno kisha laza kidogo mswaki na tengeneza nyuzi 45 kama mchoro huu unavyoonyesha.

utakuwa unapiga mswaki kuelekea juu na chini, ukihakikisha mswaki wako unafikia kila jino kadiri ya maelezo yanayofuata hapa chini.

Njia sahihi ya kupiga mswaki ni kwa kufuata mpangilio fulani utakaokuwezesha kukumbuka kwa urahisi kama ifuatavyo

  • Safisha sehemu ya nje ya meno ya juu, anza meno ya mwisho mfano kutoka kulia, kisha meno ya mbele, halafu meno ya kushoto. Kisha hamia upande wa meno ya chini, anzia upande huo ulio malizia (kushoto) kisha piga meno ya mbele kisha ya kulia.
  • Hamia upande wa ndani pale ulipomalizia upande wa kulia safisha sehemu ya ndani ya meno ya meno ya juu, kisha ya mbele, kisha ya upande wa kushoto. Hamia upande wa meno ya chini ukianzia ulikomalizia (kushoto), kisha meno ya mbele, kisha meno ya kulia
  • Safisha na sehemu ya kutafunia kwa meno yote juu na chini (fuata mzunguko kama maelezo hapo juu)
  • Safisha na ulimi wako kwa kutumia mswaki, toa ulimi nje ili uweze kufika sehemu ya nyuma ya ulimi. Fanya kwa utaratibu na kama utapata msukumo wa kutaka kutapika acha kwanza tulia halafu rudia tena kusafisha.

2. UZI WA KUSAFISHA KATI YA MENO (DENTAL FLOSS)

Huu ni uzi maalumu kwa ajili ya kusafisha kati ya meno, sehemu ambayo brashi za mswaki haziwezi kufika. Huondoa mabaki ya chakula na ugavu kati ya meno na kwenye fizi. Sehemu hizi zisipotunzwa vizuri hupelekea bacteria kusababisha ugonjwa wa kuoza kwa meno, ugonjwa wa fizi, na pia harufu mbaya mdomoni. Matumizi ya uzi wa kusafishia meno yanashauriwa kufanyika mara moja kila siku, hasa wakati wa usiku kabla ya kupiga mswaki.

Namna ya kutumia uzi wa kusafisha meno

Kata kipande cha uzi kiasi cha sentimeta 46 – 51. Zungusha upande mmoja kwenye kidole cha katikati cha mkono wa kushoto na upande mwingine katika kidole cha kati cha mkono wa kulia, mpaka ufikie mbali wa sentimeta 5-8 kati ya mkono wa kulia na wa kushoto. Angalia mchoro ufuatao

 

Anza kusafisha kati ya meno mpaka kwenye ufizi. Kunja uzi wa kusafishia kuzunguka jino kuelekea upande mmoja kutengeneza herufi U, kisha usukume taratibu mpaka unapita kwenye ufizi.

 

Tembeza uzi huo juu na chini mara kadhaa ukiwa umebanwa kuelekea jino husika kusafisha ugavu sehemu hiyo ya jino. Kumbuka kupitisha uzi wa kusafisha kati ya meno bila kuubana upande wa jino husika, haitaondoa ugavu vizuri, na unaweza kuumiza fizi zako. Fuata mzunguko maalumu kwa kuanzia juu upande wa kulia, safisha sehemu zote za kati kati ya meno, endelea mpaka upande wa kushoto, kisha hamia upande wa chini kuanzia ulipomalizia (kushoto), kisha zunguka mpaka upande wa kulia. kusafisha kwa kutumia uzi mwanzoni itaweza kuchukua muda zaidi, ila ukizoea utatumia muda wa dakika moja.

3.VIJITI VYA KUCHOKONOA KATI YA MENO (TOOTHPICK)

Vijiti vya kuchokonoa kati ya meno, vinaweza kuwa na umbo la mzunguko au bapa, hutengenezwa kwa mbao au plastiki. Pia vinaweza kuwekewa ladha kwenye ncha. Hutumika kuondoa mabaki ya chakula yaliyojishika kati ya meno

Matumizi sahihi ya vijiti vya kuchokonoa kati ya meno

Vijiti hivi vinashariwa kutumiwa na watu wenye meno yenye nafasi ya kupitisha vijiti hivi kwa urahisi. Tumia kijiti hiki taratibu, kuchokonoa mabaki makubwa ya chakula kati ya meno, bila kuharibu fizi zako. Matumizi ya mara kwa mara na kutumia nguvu ya vichokonoleo hivi inaweza kusababisha ufizi kusinyaa na kuacha nafasi pia kupelekea meno kupata ganzi (sensitivity).

Faida za uzi wa kusafishia na vijiti vya kuchokonoa kati ya meno

Vijiti vya kuchokonolea kati ya meno, na uzi wa kusafisha kati ya meno, vinaweza kufika mahali ambapo brashi za mswaki haziwezi kufika. Uchafu ukikaa maeneo haya bila kutolewa huweza kuoza, kutoa harufu mbaya na pia kuwezesha bakteria wanaoozesha meno na wanaosababisha ugonjwa wa fizi waongezeke kwa wingi. Matumizi ya vitu hivi huweza kusaidia kudhibiti tatizo la mabaki ya chakula na ugavu kati ya meno.

Kumbuka

Matumizi ya vijiti vya kuchokonelea kati ya meno, hayawezi kuchukua nafasi ya matumizi ya uzi wa kusafisha kati ya meno. Vichokonoleo hivi hutumiwa tu kutoa mabaki ya chakula kilichobana kati ya meno baada ya kula, na meno yenye nafasi ya kutosha kuruhusu vichokonoleo hivi kupita kwa urahisi.

Muda

Hakuna muda maalumu unaoshauriwa wa matumizi ya vijiti vya kuchokonoa kati ya meno, unatumia pale unapohitaji. Kumbuka matumizi ya kupitiliza ya vijiti hivi huweza kuharibu fizi zako.

Free Presentantion on ...

Free Presentation on Weight Loss with Zohra ...

+ View

Recent Articles

Utastaajabishwa na ...

Wakati mwingine tunakata tamaa kufanya mambo ...

+ View

Matatizo sugu yanayo ...

Wengi wetu tunafahamu umuhimu wa mazoezi katika ...

+ View

MEN’S BELLY FAT: Pride ...

The fact that abdominal fat, or belly fat, is not ...

+ View
  • Prev
  • Sponsor this Section
Scroll to top