Reputation Management
CPR certification onlineCPR certification online

 

Kusafisha kinywa kwa usahihi kunahusisha matumizi ya

1. Mswaki

2. Uzi wa kusafisha kati ya meno (dental floss)

3. Vijiti vya kuchokonoa kati ya meno

Read more ...

 

Picha hii ya mzee Juma Kulwa Kuliwa miaka michache kabla hajapata tatizo hilo la kiafya

Mzee Juma Kulwa Kuliwa (1950) ni mkazi wa Tabora, alipata ugonjwa uliopelekea kufanyiwa operesheni kubwa kuondoa sehemu ya taya la juu iliyokuwa imeharibika kwa ugonjwa unaoitwa “Osteomyelitis”. Ugonjwa huu huharibu mfupa na matibabu yake yanategemea na usugu wa tatizo, huweza kuhusisha matumizi ya dawa ya kuua bakteria (antibiotics) pekee, au pamoja na upasuaji wa kuondoa sehemu ya mfupa iliyoharibika. Mzee Kulwa alifanyiwa upasuaji na kuondolewa sehemu ya taya la juu. Baada ya matibabu haya alipata changamoto ya kula na kuongea na thamani ya maisha ilikuwa duni sana (reduced quality of life). Hata hivyo baada ya wataalamu kumtibu sasa, imemrudishia thamani yake ya mwanzo. Hili hapa simulizi lake

Read more ...

MAMBO YA KUZINGATIA KABLA NA BAADA YA KUNG'OA JINO

Imehaririwa na Dr Arnold Augustino Mtenga D.D.S., MDent (Daktari bingwa wa upasuaji wa afya ya kinywa Hospitali ya Taifa Muhimbili)

Meno ni sehemu ya mwili ambayo hufanya kazi kubwa ikiwemo kutafuna chakula, kuongea, na kuboresha muonekano. Kwa kawaida kuna meno ya aina mbili, ya utoto ambayo huanza kuota umri wa wastani wa miezi sita, na meno ya ukubwa ambayo nayo huanza kuota wastani wa miaka sita na kuendelea. Meno hujishika kwenye mfupa maalumu ulioko kwenye taya. Meno kama sehemu nyingine ya mwili yasipotunzwa vizuri yanaweza kushambuliwa na ugonjwa wa kuoza, au ugonjwa wa fizi ambao hushambulia sehemu ambayo jino limejishika.

Kuna msemo wa Kiswahili unaosema dawa ya jino linalouma ni kungoa. Jambo hili limepelekea watu wengi wakienda hospitali wanasema nimekuja kuongoa jino. Ni vizuri kujua kuwa matibabu ya jino lenye tatizo lolote yapo, na kungoa huwa ni jambo la mwisho kabisa. Tuangalie sababu zinazoweza kupelekea daktari wa afya ya kinywa na meno ashauri jino kung’olewa.

Read more ...

 

    

picha hizi zinaonyesha kabla ya matibabu ya mapengo

    

picha hizi zinaonyesha baada ya matibabu ya mapengo

Imehaririwa na Dr Lorna Carneiro D.D.S., PhD., (Mhadhiri MUHAS na Daktari Bingwa wa Meno bandia - Prosthodontists)

Mapengo ni tatizo linalotokana na kupoteza jino moja au zaidi. Mapengo hasa meno ya mbele, hupunguza kujiamini na huweza kumfanya mtu kuwa na aibu mbele za watu, au kumfanya asipende kujichanganya kwenye shughuli zinazohusisha watu wengi. Pamoja na kuichukia hali hii, kuna wengine hawafahamu kama mapengo yanaweza kutibiwa. Binadamu huwa ana aina mbili za meno, ya utotoni na a ukubwani.

Read more ...

Free Presentantion on ...

Free Presentation on Weight Loss with Zohra ...

+ View

Recent Articles

Are you looking for ...

We are a team of doctors, medical writers, health ...

+ View

Lishe bora ni dawa

Kama kuna kitu muhimu na cha msingi sana ambacho ...

+ View

Huu hapa mpangilio wa ...

  Mwaka mmoja kabla ya kumaliza shahada yangu ya ...

+ View
  • Prev
  • Sponsor this Section
Scroll to top